Edward Teller
From Wikipedia, the free encyclopedia
Edward Teller (1908 - 2003) alikuwa mwanafizikia wa Hungaria. Anajulikana kama baba wa bomu la hidrojeni. Hata hivyo hakupenda hiyo sifa ya kuwa ndiye mvumbuzi wa bomu la hidrojeni. Maishani mwake Edward Teller anasemekana kuwa mwenye talanta kuu katika uwanja wa fizikia. Hata hivyo anajulikana pia kwa kuwa mtu mgumu sana wa kuelewana naye.