Kaya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kaya (kwa Kiingereza household) ni kundi la watu wanaoishi mahali pamoja kama familia. Kwa maana nyingine ni nyumba wanapoishi.
Istilahi hiyo inayotumiwa katika takwimu za watu, kwa mfano wakati wa sensa. Ufafanuzi wa kawaida ni "watu wanaokaa pamoja na kula pamoja". Mjini kaya inaweza kukaa katika chumba kimoja. Mashambani inawezekana kuna familia inayokalia kwa pamoja vyumba kadhaa vya jirani. Kwa maana ya takwimu kaya inaweza kuwa hata mtu mmoja tu akiishi peke yake.