Malaysia Mashariki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Malaysia Mashariki ("Malaysia Timur") ni sehemu ya Malaysia inayopatikana kaskazini mwa kisiwa cha Borneo na visiwa vidogo vya jirani.
Inaundwa na majimbo ya Sarawak na Sabah pamoja na eneo la shirikisho la Labuan (funguvisiwa) lililoanzishwa mwaka 1984.
Idadi ya wakazi ilikuwa milioni 5.77 mwaka 2010.
Upande wa dini, Waislamu ni 51.3%, Wakristo 33.3%, Wabuddha 9.3% n.k.