Mtumiaji:Kipala/Bonde la Fergana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bonde la Fergana ni bonde katika Asia ya Kati linaloenea mashariki mwa Uzbekistan, kusini mwa Kyrgyzstan na Tajikistan kaskazini.
Bonde hili linapata umuhimu waka likiwa eneo lenye maji na rutba linaloweza kulisha watu wengi kiasi katika mazingira yabisi ya Asia ya Kati. Tangu nyakati za kale lilikuwa mahali ambako makabila, mataifa na tamaduni mbalimbali zilikutana na kuishi pamoja.
Bonde lina umbo la pembetatu lilipokea rutba kutokana kwa mito inayotelemka kutoka milima ya karibu ambayo ni Tienshan na Alai ambao ni mito ya Naryn na Kara Darya inayoungana kuunda mto mto wa Syr Darya. Habari za historia ya bonde hilo zinaanzia zaidi ya miaka 2,300 iliyopita.