Jumapili, 14 Des 2025
Remove ads
Most read


Tanzania
nchi ya Afrika Mashariki
Tanzania ni nchi iliyopo Afrika ya Mashariki, ndani ya ukanda wa maziwa makuu ya Afrika. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa kaskazini, Bahari ya Hindi upande wa mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi na Rwanda upande wa magharibi. Eneo la Tanzania ni takriban kilometa za mraba 947,303. Eneo linalokaliwa na maji ni asilimia 6.2. Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika, upo kaskazini-mashariki mwa Tanzania. Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 ilikuwa 61,741,120. Msongamano wa watu ni 47.5 kwa km².
Mji mkuu ni Dodoma
192 views


Nigeria
Nigeria pia Nijeria, rasmi kama Jamhuri ya Shirikisho ya Nigeria ni nchi iliyoko Magharibi mwa Afrika. Inapakana na Benin upande wa magharibi, Niger upande wa kaskazini, Chad na Kameruni upande wa mashariki, na upande wa kusini na Bahari ya Atlantiki. Ikiwa na idadi ya watu milioni 232 ndio nchi ya sita kubwa duniani kwa idadi ya watu na ni nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika. Abuja ndiyo mji mkuu, huku Lagos ikiwa jiji kubwa zaidi.
188 views


Burundi
nchi huru barani Afrika
Burundi, kirasmi Jamhuri ya Burundi, ni nchi ndogo ambayo iko katika eneo la Maziwa Makubwa ya Afrika. Burundi imepakana na Rwanda upande wa kaskazini, Tanzania upande wa mashariki, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi.Ina idadi ya watu takriban milioni 13 ikiwa nchi ya 78 kubwa kwa idadi ya watu. Mji mkuu ni Gitega na mji mkubwa ni Bujumbura. Burundi ni mwanachama wa Umoja wa Afrika na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
188 views


Nikaragua
Nikaragua ni nchi ya Amerika ya Kati inayopakana na Honduras kaskazini, Kosta Rika kusini, Bahari ya Pasifiki magharibi, na Bahari ya Karibi mashariki. Ina idadi ya watu takriban milioni 6.36 kwa makadirio ya mwaka 2023. Managua ndiyo mji mkuu na jiji kubwa zaidi. Eneo lake ni takribani kilomita za mraba 130,370. Nikaragua imegawanywa katika mikoa 15 na mikoa miwili ya kujitawala katika pwani ya Karibi. Lugha rasmi ni Kihispania, huku Krioli ya Kiingereza, Kimiskito, Kirama, na Kisumo zikitumika katika maeneo ya pwani. Inajulikana kwa maziwa makubwa, milima ya volkeno, na urithi wake wa Kihispania uliochanganyikana na tamaduni za wenyeji.
187 views
Show more




