![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/4a/Izmir_coast.jpg/640px-Izmir_coast.jpg&w=640&q=50)
İzmir
From Wikipedia, the free encyclopedia
İzmir, kwa jina la kihistoria Smyrna, ni mji wa tatu kwa ukubwa katika Uturuki, na ndio mji wenye bandari kubwa baada ya Istanbul. Upo katika eneo la maji yatokayo Ghuba ya İzmir, katika Bahari ya Aegean.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/4a/Izmir_coast.jpg/640px-Izmir_coast.jpg)
Huu ni mji mkuu wa Mkoa wa İzmir, ambao una eneo la kilomita za mraba zipatazo 7350.
Mji wa İzmir una wilaya zipatazo kumi. Wilaya hizo ni pamoja na Balçova, Bornova, Buca, Çiğli, Gaziemir, Güzelbahçe, Karşıyaka, Konak, Menemen, na Narlıdere, ambazo kila moja ni tofauti sana na nyingine.
Kanisa la Smirna ni kati ya yale saba ambayo yaliandikiwa barua katika Ufunuo wa Yohane, kitabu cha mwisho cha Agano Jipya na cha Biblia ya Kikristo. Ndilo linalosifiwa zaidi, hasa kutokana na kiongozi wake, askofu Polikarpo wa Smirna.