Aust-Agder
From Wikipedia, the free encyclopedia
Aust-Agder ni moja kati ya Majimbo ya Norwei (fylke). Imepakana na Telemark, Rogaland, na Vest-Agder. Kunako mwaka wa 2002, kulikuwa na wakazi takriban 102,945, ambayo ni 2.2% ya jumla ya idadi ya wakazi wa nchini Norwei. Ni kweli ina kilomita za mraba zupatazo 9,212 (3,557 sq mi). Kitovu cha utawala wa jimboni hapa ni mjini Arendal.
Jimbo, ambalo lipo katika pwani ya Skagerrak, linatoka Gjernestangen hadi Risør hadi Kvåsefjorden hadi Lillesand. Sehemu za ndani za maeneo yake ni pamoja na Setesdalsheiene na Austheiene. Takriban 77% ya wakazi wake wanaishi katika eneo la pwani, ambapo ndipo kuna ujenzi mkubwa kabisa. Utalii ni muhimu mjini hapa, kama jinsi ilivyo Arendal na miji mingine ya pwani ni vivutio maarufu.
Jimbo hili linajumuisha kisiwa cha Tromøy, Justøya, na Sandøya. Ndani ya jimbo linajumuisha wilaya ya Setesdal, kupitia mto Otra unaomwagikia baharini.