Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (kwa Kiingereza Tanzania Episcopal Conference, TEC) ni muundo wa Kanisa Katoliki unaokutanisha maaskofu wake wote wa nchi ya Tanzania, wakiwa wanaongoza jimbo, au ni waandamizi, wasaidizi au wamestaafu.
Maelezo zaidi Imani, Muundo ...
Funga
Katiba ya Baraza ilipitishwa na Ukulu mtakatifu tarehe 8 Januari 1980.
Makao makuu yako Dar es Salaam, mtaa wa Kurasini, lakini kuna mpango wa kuyahamishia Dodoma, mji mkuu wa nchi.
TEC ni kiungo cha Association of Member Episcopal Conferences in Eastern Africa (AMECEA) na cha Symposium of Episcopal Conferences of Africa and Madagascar (SECAM).