Kazan wa Japani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kazan (29 Novemba, 968 – 17 Machi, 1008) alikuwa mfalme mkuu wa 65 (Tenno) wa Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Morasada, na alikuwa mwana wa kwanza wa Tenno Reizei. Mwaka wa 984 alimfuata mjomba wake, Tenno En'yu, na kuwa mfalme hadi kujiuzulu mwaka wa 986. Aliyemfuata kama Tenno ni binamu yake, Ichijo. Baadaye mdogo wake, Sanjo, pia alikuwa Tenno.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/b/bb/Tenn%C5%8D_Kazan_detail.jpg/220px-Tenn%C5%8D_Kazan_detail.jpg)