Kikyrili
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kisirili ni aina ya mwandiko au alfabeti inayotumiwa kuandika lugha mbalimbali za Ulaya ya Mashariki na Asia ya Kati, kwa mfano Kirusi, Kiserbia, Kitajiki.
Jina limetokana na mmonaki na mtalaamu Mgiriki Mt. Kyrilo (827 - 14 Februari 869) aliyesemekana aliunda namna hiyo ya mwandiko kwa ajili ya lugha za Kislavoni pamoja na mdogo wake Mt. Methodio.