Kitelugu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kitelugu ni lugha ya Kidravidi nchini Uhindi inayozungumzwa na Watelugu. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kitelugu nchini Uhindi imehesabiwa kuwa watu sabini na tatu milioni na laki nane. Pia kuna wasemaji 600 nchini Singapuri. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kitelugu iko katika kundi lake lenyewe la Kitelugu.