Kleri
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kleri ni kundi la watu wanaoongoza dini fulani. Jina linatokana na neno la Kigiriki "κλῆρος" - klēros, "bahati", "sudi" au also "urithi".
Katika madhehebu mengi ya Ukristo kleri ina daraja takatifu tatu: kuanzia juu ni uaskofu, upadri na ushemasi. Hata hivyo baadhi yao wanapewa pia majina mengine kulingana na huduma zao, kwa mfano: Papa, kardinali, monsinyori, abati, kanoni, arkimandrita n.k.
Katika Uislamu hakuna ukuhani, hivyo uongozi unategemea tu elimu ya dini: kuna mufti, imamu, ustadhi n.k.