Korporale
From Wikipedia, the free encyclopedia
Korporale (kwa Kiingereza: corporal) ni kitambaa aghalabu cheupe kidogo cha mraba ambacho kinatandikwa altareni juu ya vitambaa vingine vyote na ambapo juu yake huwekwa patena, kikombe na pengine sibori katika adhimisho la Misa.
Jina asili la Kilatini: corporax linatokana na neno corpus, yaani mwili, kumaanisha kwamba lengo lake ni hasa kubeba Mwili wa Kristo katika ekaristi.