Kutoka (Biblia)
kitambo kitabu Biblia, mchanganyiko 40 sura ya / From Wikipedia, the free encyclopedia
Kitabu cha Kutoka ni kitabu cha pili katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), na kwa hiyo pia katika Agano la Kale (sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo); kitabu cha kwanza ni Mwanzo.
Kwa asili kimeandikwa kwa Kiebrania, na katika lugha hiyo kinaitwa שמות, Shemot, maana yake “majina”, kutokana na neno lake la kwanza.
Wengine wanakiita Kitabu cha Pili cha Mose (au Musa) kwa vile inafikiriwa kuwa ndiye mwandishi wa kitabu hicho. Kwa lugha ya Kiyunani, kinaitwa ἔξοδος, Exodos, maana yake “kuondoka kwa watu wengi pamoja”.
Kitabu cha Kutoka kina sura arobaini.
- Sura 1 hadi 18 zinasimulia Waisraeli walivyokombolewa na Mungu kutoka utumwani kule Misri na walivyosafiri mpaka Mlima Sinai.
- Sura 19 hadi 24 zinasimulia Mungu alivyofanya nao agano pamoja na kuwapa mwongozo wa maisha (Amri Kumi na maagizo mengine).
- Sura 25 hadi 31 zinaeleza utengenezaji wa hema takatifu (au hema la mkutano) na Sanduku la Agano.
- Sura 32 hadi 34 zinahadithia Waisraeli walivyoasi na kuabudu sanamu ya ndama wakati Mose alipokuwa amekwenda kuzungumza na Mungu mlimani Sinai.
- Hatimaye, sura 35 hadi 40 zinaeleza maagizo mengine kuhusu hema takatifu.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.