![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e1/MEP_symbol.jpg/640px-MEP_symbol.jpg&w=640&q=50)
Misheni za Paris
From Wikipedia, the free encyclopedia
Misheni za Paris (kwa Kifaransa: Missions Etrangères de Paris kifupi M.E.P., kwa Kilatini: Societas Parisiensis missionum ad exteras gentes) ni jumuiya ya wamisionari Wakatoliki kwa ajili ya misheni katika nchi za Asia .
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e1/MEP_symbol.jpg/320px-MEP_symbol.jpg)
Katika utaratibu wa sheria za Kanisa la Kilatini ni shirika la maisha ya kitume lenye hadhi ya Kipapa na liko chini ya Idara ya Uinjilishaji wa Mataifa.
Lilianzishwa mwaka 1658 likafanya kazi hasa Asia Mashariki, na hadi sasa ndiko liliko na wamisionari wengi, mbali ya Ufaransa na Madagaska. Duniani kote ni 198, kati yao mapadri 184.