Mkondo wa bahari
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkondo wa bahari ni mwendo mfululizo wa maji ndani ya bahari. Ni kama mto ndani ya bahari. Maji ya mkondo huwa na halijoto tofauti na maji ya mazingira.
Kwa kawaida huwa mikondo ya bahari yahusu maji karibu na uso wa bahari. Kwa hiyo kama mto wa kawaida mkondo una kimo chake vile vile na maji yake hutembea juu ya maji ya chini. Kuna pia mikondo ya chini.
Nguvu inayosukuma maji si mtelemko na nguvu ya uvutano jinsi ilivyo kwa mito ya nchi kavu bali kani mbalimbali kama mazunguko ya dunia, upepo, halijoto ya eneo na tofauti za kiwango cha chumvi ndani ya maji kieneo.