Karitoni wa Souka
From Wikipedia, the free encyclopedia
Karitoni wa Souka (Konya, leo nchini Uturuki karne ya 3 - karibu na Bethlehemu, Palestina, 350 hivi) alikuwa Mkristo ambaye, baada ya kuteswa ujanani kwa imani yake, akawa mmonaki ambaye alianzisha monasteri kadhaa jangwani[1][2][3][4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yao ni tarehe 28 Septemba[5][6].