Mtumiaji:Muddyb/Mohamed Bouazizi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tarek el-Tayeb Mohamed Bouazizi (Kiarabu: محمد البوعزيزي; 29 Machi 1984 – 4 Januari 2011) alikuwa mfanyabiashara mdogomdogo (mmarufu mmachinga) kutoka nchini Tunisia ambaye amejiwasha moto mnamo tarehe 17 Desemba 2010, hali iliyoleta taharuki na hatimaye Mapinduzi ya Tunisia na baadaye kupamba moto kwa Vuguvugu la Uarabuni dhidi ya tawala za kiimla na kidhalimu. Kujitoa kwake kafara, ni tokeo la kuporwa vyombo vyake vya kazi, manyanyaso na masakamo yaliyokuwa yanaelekezwa kwake kutoka kwa polisi wa manishapaa na kikosi chake.
Muddyb/Mohamed Bouazizi | |
---|---|
Amezaliwa | Tarek al-Tayeb Mohamed Bouazizi[1] (1984-03-29)29 Machi 1984 |
Amekufa | 4 Januari 2011 (umri 26) Ben Arous, Tunisia |
Sababu ya kifo | Majelaha ya moto yaliyotoka na kujitoa kafara |
Amezikwa | Makaburi ya Garaat Bennour |
Majina mengine | Basboosa |
Kazi yake | Mmachinga |
Anajulikana kwa ajili ya | Kujitoa kafara |
Jazba kutoka kwa wananchi zilipamba moto baada ya kifo cha - Bouazizi, jambo ambalo lilipelekea rais wa wakati huo Zine El Abidine Ben Ali kujiuzuru wadhifa wake kama rais wa nchi mnamo tarehe 14 Januari 2011, baada ya kudumu madarakani kwa takriban miaka 23. Kufanikiwa kwa maandamano ya Tunisia yamevutia nchi nyengine kadhaa za Kiarabu na zile ambazo si za Kiarabu kufanya migomo na maandamano dhidi ya tawala dhalimu. Maandamano haya yaliambatana na watu wengine waliojitoa kafara kwa kufuatia kitendo cha Bouazizi kujitia moto, ikiwa thubutu la kutaka kuuangusha serikali za kiutawala wa kimabavu na kidhalimu. Watu hao na Bouazizi walisifiwa na watoa maoni wa Kiarabu wakiwahesabia kama "mashujaa wafiadini wa mapinduzi ya Mashariki ya Kati mpya".[2]
Mwaka wa 2011, Bouazizi na wenzie wanne walipewa tuzo za Sakharov Prize kwa mchango wao wa "mabadiliko ya kihistoria katika Ulimwengu wa Kiarabu" (tuzo zimetolewa baada ya kifo chao).[3] Serikali ya Tunisia imemuenzi kwa muhuri wa posta wenye sura ya Bouazizi.[4] Gazeti la kila siku la Uingereza - The Times wamemuita Bouazizi kama "Mtu Maarufu wa 2011".[5][6]