Ushairi
muundo / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ushairi ni utungo wa kisanaa ulio na madhumuni ya kutumbuiza au kuelimisha. Tena, ushairi ni tawi mojawapo la fasihi andishi. Kinyume chake ni nathari.[1]
Inawezekana kutunga mashairi yenyewe au kutumia lugha ya kishairi katika aina nyingine za sanaa, kwa mfano tamthiliya au nyimbo.
Ushairi una historia ndefu. Kwa mfano, mwanafalsafa Aristotle katika kitabu chake Ushairi ("Poetics" kwa Kiingereza) anachunguza matumizi yake katika hotuba, tamthiliya, nyimbo na futuhi.
Ushairi una vipera vifuatavyo:
1. nyimbo
2. ngonjera
3. mashairi mepesi
4. maghani
5. tendi
6. rara
7. rara nafsi