From Wikipedia, the free encyclopedia
Nabii Baruku mwana wa Neria (kwa Kiebrania ברוך בן נריה) alikuwa mwandishi wa karne ya 6 KK, maarufu kama karani, mwanafunzi na rafiki mpendwa wa nabii Yeremia.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu na madhehebu mbalimbali ya Ukristo.
Kadiri ya Yosefu Flavius, alikuwa sharifu wa Uyahudi, mwana wa Neria na ndugu wa Seraia mwana wa Neria, waziri wa mfalme Zedekia wa Ufalme wa Yuda.[1][2]
Baruku aliandika maneno ya Yeremia alivyoagizwa naye[3] akabaki mwaminifu kwake hata katika dhuluma. Yeremia alipokuwa mafichoni alimtuma kusoma katika Hekalu la Yerusalemu utabiri wa adhabu dhidi ya mfalme Yehoyakimu [4] Huenda kama shukrani kwa kutekeleza agizo hilo gumu, Yeremia alimtabiria mema.[5]
Wote wawili walishuhudia maangamizi ya Yerusalemu (587 KK) wakabaki pamoja baada yake[6][7][8]mpaka walipopelekwa nchini Misri.
Uhusiano huo ulifanya Baruku aheshimiwe sana na vizazi vilivyofuata, hata vitabu viliandikwa kwa jina lake:
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.