Nabii Eliya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Eliya (kwa Kiebrania אליהו, Eliyahu, maana yake "YHWH ndiye Mungu wangu";[1] kwa Kiarabu إلياس, Ilyās), alikuwa nabii katika Ufalme wa Israeli wakati wa wafalme Ahabu na Ahazia (karne ya 9 KK).
Habari za nabii huyo maarufu sana katika Biblia, na labda katika Qurani pia, zinapatikana hasa katika vitabu vya Wafalme.
Dhidi ya uasi wa taifa la Mwenyezi Mungu, alitetea haki za Mungu pekee kwa ari kubwa hivi kwamba watu waliwafananisha naye Yohane Mbatizaji na hata Yesu mwenyewe[2].
Hakuacha maandishi, lakini kumbukumbu yake inatunzwa vizuri sana, hasa katika Mlima Karmeli.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.