Nikita Krushchov
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nikita Sergeyevich Krushchov (Kirusi: Ники́та Серге́евич Хрущёв - Nikita Sergeyevich Khrushchyov) (17 Aprili 1894 – 11 Septemba 1971) alikuwa kiongozi wa Umoja wa Kisovyeti baada ya kifo cha Joseph Stalin. Alitawala kati ya 1953 hadi 1964.
Krushchov alizaliwa mjini Kalinovka, Urusi. Baadaye alihamia Ukraine. Alikuwa mfanyakazi wa migofi akajiunga na chama cha Bolsheviki.
Alipanda ngazi chini ya Stalin. Baada ya kifo chake akawa kiongozi aliyemfuata. Cheo chake kilikuwa "Mwenyekiti wa chama cha kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti" lakini alikuwa na madaraka kumshinda aliyekuwa na cheo cha rais wa nchi.
Mwaka wa 1964 aliondolewa madarakani na mfuasi wake Leonid Brezhnev.