Nordland
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nordland ni moja kati ya Majimbo ya Norwei. Jimbo lipo katika kanda ya Kaskazini mwa Norwei, imepakana na Troms kwa upande wa kaskazini, Nord-Trøndelag kwa upane wa kusini, Norrbottens län nchini Sweden kwa upande wa mashariki, Västerbottens län kwa upande wa kusini-mashariki, na Bahari ya Atlantiki (Bahari ya Norwei) kwa upande wa magharibi. Awali jimbo lilikuwa likijulikana kama Nordlandene amt. Makao makuu ya jimbo yapo mjini Bodø. Kisiwa cha barafu cha Jan Mayen kimekuwa chini ya Nordland tangu 1995.
Katika upande wa kusini mwa Vega, -meorodheshwa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya Unesco. Historia ya Nordland ni ngano kuhusu zawadi zitokanazo na bahari: Ni moja ya sehemu inayotoa mazalia mengi yanayotokana na bahari katika dunia na imekuwa ikitoa chakula tangu enzi za kale, bahari hiyohiyo inayotengeneza tabia-nchi ya wastani kuliko mahali popote pale katika eneo la barafu.