From Wikipedia, the free encyclopedia
Nyanda za juu za Adamawa (kwa Kiingereza: Adamawa Plateau; Kifaransa: 'Massif de l'Adamaoua') ni eneo la Afrika ya Kati linalopatikana kuanzia kusini-mashariki mwa Nigeria kupitia kaskazini mwa Kamerun (mikoa ya Adamawa na Kaskazini) hadi Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Jina la nyanda za juu hizo lilitolewa kwa kumbukumbu ya kiongozi Mwislamu wa Wafulani, Modibo Adama. Sehemu yake nchini Nigeria inajulikana pia kama Milima ya Gotel.
Nyanda za Juu za Adamawa ndizo chanzo cha mito mingi, pamoja na Mto Benue. Ni muhimu kwa madini yake ya boksiti. [1] Mwinuko wa wastani ni kama mita 1,000, [2] lakini mwinuko unaweza kufikia urefu wa mita 2,650. Uoto ni hasa savana, watu wanaoishi hapa ni wachache. Ufugaji wa ng'ombe ni kazi kuu katika eneo hilo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.