Pasaka
From Wikipedia, the free encyclopedia
Pasaka ni sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo. Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania "פסח" (tamka: pasakh).
- Pasaka ya Kiyahudi ni ukumbusho wa ukombozi wa Wanaisraeli kutoka Misri wakati wa Musa mnamo miaka ya 1200 KK.
- Pasaka ya Kikristo ni ukumbusho wa kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulubiwa kwake, mnamo Aprili 30. Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika Ukristo.
Taarifa za Agano Jipya zinatoa habari ya kuwa kufa na kufufuka kwa Yesu yametokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi. Kwa hiyo jina la sikukuu hiyo limeendelea kutumika kwa ajili ya sherehe ya Kikristo.