Polima
From Wikipedia, the free encyclopedia
Polima (kutoka Kiingereza "polymer") ni molekuli ndefu iliyotengenezwa kwa kuungana pamoja vizio vingi vidogo vya kemikali.
Jina polima linatokana na neno ambalo ni la Kigiriki cha kisayansi lililopatikana kwa kuunganisha πολύ poli ‘nyingi‘ na μέρος meros ‘sehemu, kizio‘ kwa hiyo kumaanisha "ya vizio vingi". Hii inaonyesha jinsi muundo wa polima unavyokuwa na vizio vingi vidogo vilivyounganishwa pamoja kuwa molekuli kubwa.
Mmenyuko wa kikemia unaounganisha vizio vya kemikali kuunda polima huitwa upolimishaji.