Safu ya milima
From Wikipedia, the free encyclopedia
Safu ya milima ni msururu wa milima iliyokaribiana[1]. Milima hiyo hutenganishwa na nyanda za juu au mabonde.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/9d/Aberdare_National_Park_Wikivoyage_Banner.jpg/220px-Aberdare_National_Park_Wikivoyage_Banner.jpg)
Mifano ya safu za milima ni kama vile, Safu ya Aberdare, Milima Atlas, Alpi na Himalaya. Safu nyingi za milima duniani zilitokea kama milima kunjamano.