San Salvador
From Wikipedia, the free encyclopedia
San Salvador ni mji mkuu wa El Salvador katika Amerika ya Kati pia mji mkubwa wa nchi hii mwenye wakazi 485,847 (2001) ambao ni theluthi moja wa watu wote nchini.
Jina la mji lamaanisha "Mtakatifu Mwokozi" kwa Kihispania likimaanisha Yesu Kristo.
San Salvador iko kwenye kimo cha m 668 juu ya UB. Imeathiriwa mara kwa mara na mitetemeko ya ardhi.