Sikipi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Sikipi ni ndege wa jenasi mbalimbali katika nusufamilia Perdicinae wa familia Phasianidae. Spishi za Ptilopachus huainishwa katika familia Odontophoridae siku hizi, kwa sababu zina nasaba na tombo wa Dunia Mpya. Ndege hawa wanafanana na kwale na tombo, lakini ukubwa wao ni katikati ya zile za ndege hawa. Hata mwenendo wao ni kama ule wa ndege hawa. Hula mbegu hasa lakini wadudu pia. Hutaga mayai tano hadi zaidi ya kumi ardhini pengine juu ya manyasi makavu.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Sikipi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Sikipi wa Afrika | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 13 za sikipi:
| ||||||||||||
Funga
Sikipi wanatokea Afrika, Ulaya na Asia, lakini sikipi chukar amewasilishwa katika Amerika ya Kaskazini, New Zealand na Hawaii. Spishi nyingi huwindwa sana mahali pengi.