Tana (ziwa)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ziwa la Tana ni ziwa kubwa la Ethiopia ambalo ni asili ya Nile ya Buluu. Beseni lake liko takriban km 370 kaskazini-magharibi kwa Addis Ababa katika nyanda za juu za Ethiopia.
Ukweli wa haraka Ziwa Tana ...
| |
Mahali | Nyanda za juu za Ethiopia, (Afrika ya Mashariki) |
Eneo la maji | 2.156 km² |
Kina cha chini | 14 m |
Mito inayoingia | Rib na Gumara |
Mito inayotoka | Abbai (Nile ya buluu) |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
1.788 m |
Miji mikubwa ufukoni | Bahir Dar |
Funga
Umbo la ziwa limebadilika katika karne iliyopita kutokana na mashapo. Kamusi ya mwaka 1888 ilitaja kina cha mita 100, lakini leo ni mita 14 pekee. Eneo la ziwa hubadilika na majira ya mvua au ukame yaani kuwa na maji mengi au kidogo.
Mito mingi inaingia ziwani ikiwa mikubwa, kati yake ni mito ya Reb na Gumara.
Mto Abbai (jina la Kiethiopia la Nile ya buluu) unatoka katika ziwa.
Eneo la Ziwa la Tana ni kitovu cha kihistoria cha Ethiopia ya Kikristo. Katika visiwa vidogo ziwani kuna makanisa na monasteri 20 zilizojengwa tangu karne ya 14 BK.