Teknolojia ya Akamai
Kampuni ya kiteknologia ya Amerikani / From Wikipedia, the free encyclopedia
Akamai Technologies ni kampuni ya Marekani inayojihusisha na utoaji huduma ya mtandao hivi kwamba unapotembelea wavuti fulani, waweza kufikia faili unazotaka kwa urahisi zaidi kana kwamba seva ya wavuti hiyo iko karibu na ulipo. Teknolojia hii huitwa content delivery network (CDN). Kampuni hii ina makao makuu huko Cambridge, Mashachuttes, Marekani.
Akamai Technologies ni miongoni mwa kampuni kubwa zaidi ulimwenguni kwa kupeana huduma ya mtandao kwa kutumia program ya Akamai netsession client interface iliyoko kwa tarakilishi ya mteja. Hii kampuni imehusishwa na asilimia kati ya 15 hadi 30 ya data ipatikanayo kwa mtandao.
Mbali na hayo, Akamai Technologies ina seva kwote ulimwenguni ambapo zinginezo zimekodishwa kwa wateja wanaotaka tovuti zao zifanye kazi haraka na kwa wepesi. Unapoingia katika tovuti ya Akamai Technologies, kivinjari chako kitabadislihwa na utaelekezwa kwa moja kati ya tovuti ya hii kampuni
Akamai Technologies ilianzishwa mnamo mwaka wa 1998 na Daniel M. Lewin wakiwa pamoja na Tom Lieghton ingawapo Tom Leighton aliuawa katika shambulizi lililotukia mnamo Septemba 11 mwaka wa 2001.Leighton kwa wakati huu ndiye Mkurugenzi Mtendaji. Akamai ni jina la kihawaiii linalomaanisha ‘ujanja’ kwa maana teknolojia yao ina ujanja wa kuwasilisha wavuti kwako kwa haraka.