Tohe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Tohe ni wanyamapori wa jenasi Pelea na Redunca katika familia Bovidae. Wana rangi ya mchanga au ya kijivu lakini tumbo ni jeupe. Madume ya Redunca wana pembe zilizopindika kuelekea mbele, wale wa Pelea wana pembe nyofu. Wanatokea mahali pa nyasi nzito karibu na maji au misitu milimani (tohe-milima na tohe pembe-nyofu). Wanyama hawa hula nyasi na matete.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Tohe | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Tohe ndope (Redunca redunca) | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusufamilia 2, jenasi 2, spishi 4:
| ||||||||||||
Funga