Trevor Graham
From Wikipedia, the free encyclopedia
Trevor Graham ni mzaliwa wa Jamaika na ni kocha wa zamani wa riadha ana makao yake Marekani. Kufuatia kashfa ya BALCO, Kamati ya Olimpiki ya Marekani ilimfukuza kutoka viwanja vyao vyote vya mazoezi kwa sababu wanariadha wake kadhaa walikuwa wamepimwa na kupatikana kuwa wanatumia dawa haramu.