Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1924
From Wikipedia, the free encyclopedia
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1924 ulikuwa wa 35 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 4 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rais Calvin Coolidge (pamoja na kaimu wake Charles G. Dawes) aliwashinda mgombea wa "Democratic Party" John W. Davis (pamoja na kaimu wake Charles Bryan) na mgombea wa "Progressive Party" Robert La Follette (pamoja na kaimu wake Burton Wheeler).