Ukonfusio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ukonfusio ni mtazamo kuhusu maadili, siasa na falsafa ambao ulianzishwa na Konfusio (Kǒng Fūzǐ, or K'ung-fu-tzu, lit. "Master Kong", 551 KK–478 KK) huko China.
Mafundisho yake yalielekea kwanza siasa, lakini baadaye yalijihusisha na falsafa, hata pengine yanahesabiwa kuwa ya dini.
Baadaye mafundisho hayo yakawa rasmi nchini hadi mwanzo wa Jamhuri ya China na Jamhuri ya Watu wa China katika karne ya 20.
Nchi nyingine zilizoathiriwa sana ni Korea, Japan, Vietnam na Singapore.