![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/42/Martyrs_stadium.jpg/640px-Martyrs_stadium.jpg&w=640&q=50)
Uwanja wa michezo wa Mashahidi wa Pentekoste
From Wikipedia, the free encyclopedia
Uwanja wa Mashahidi wa Pentekoste (kwa Kifaransa: Stade des Martyrs de la PentecĂ´te, pia unajulikana kama Stade Kamanyola) ni uwanja uliopo Lingwala huko Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Unatumika hasa kwa mechi za mpira wa miguu, matamasha,na mashindano ya riadha.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/4/42/Martyrs_stadium.jpg/640px-Martyrs_stadium.jpg)
Ni uwanja wa nyumbani wa Timu ya Kitaifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, AS Vita Club na DC Motema Pembe wa Championship Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Uwanja una uwezo wa kuchukua watu 80,000 kwa mechi za kimataifa, lakini uwezo wake ni watu 125,000 kwa mechi nyingine.