Mwinda
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mwinda[1] (kwa Kiingereza: predator) kwa lugha ya biolojia ni mnyama ambaye anatumia wanyama wengine kama windo kwa kusudi la chakula; kwa kawaida kiumbehai cha windo kinauawa[2].
Kwa mfano buibui anayekamata na kula nzi ni mwinda. Vilevile kundi la simba wanaomwua na kula pundamilia ni wawinda. Nzi au pundamilia katika mifano hii ni windo.
Wanyama wawinda wengi ni walanyama, wengine walavyote, lakini si walanyama wote ni wawinda, kwa kuwa baadhi wanakula mabaki ya mizoga.
Kuna pia mimea michache ambayo inapata chakula kwa kuwinda wadudu.