Warohingya ni kundi lenye utamaduni wa Kiislamu katika Myanmar (Burma) ya magharibi linaloishi katika Dola la Rakhaing (Arakan) nchini Myanmar (Burma) hasa. Makundi mengine kutoka kwao wako pia nchini Bangla Desh. Wanaongea lugha ambalo ni karibu na Kichittagong na Kibengali.
Kwao nyumbani hawakubaliwi kama wazalendo iandaiwa ya kwamba walihamia hapa kutoka Bara Hindi hasa wakati wa Uhindi wa Kiingereza. Tangu 1983 waliondolewa uraia wa Burma. Kulikuwa na mawimbi ya mashambulio kutoka majirani yao ya Kiburma.
Mnamo mwaka 2013 takriban Rohingya 735,000 walikadiriwa wakiishi nchini Myanmar (Burma) hasa katika kaskazini ya mkoa na kwenye sehemu za pwani. Hapo ni asilimia 80-98 za wakazi. Zaidi ya milioni 1 wamekadiriwa kuishi nje ya nchi, wengi wakiwa wakimbizi.
Taasisi za kimataifa zimesema kuwa Warohingya wako kati ya vikundi wa watu wanaoteswa zaidi duniani.[1]
Mwaka wa 2015, hali ya kusikitisha ya wakimbizi Warohingya kwenye bahari ya Kihindi iliripotiwa kipana na vyombo vya habari vya kimataifa.
Yegar, Moshe (1972). Muslims of Burma. Wiesbaden: Verlag Otto Harrassowitz.
"Myanmar:The Politics of Rakhine State"(PDF). International Crisis Group. 22 Oktoba 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo(PDF) mnamo 2014-11-06. Iliwekwa mnamo 8 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Khin Maung Saw (Mei 1993). "Khin Maung Saw on Rohingya"(PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo(PDF) mnamo 2016-03-05. Iliwekwa mnamo 2015-05-17.{{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)