Yeroboamu I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yeroboamu I (kwa Kiebrania ירבעם השני au יָרָבְעָם; kwa Kigiriki Ιεροβοάμ; kwa Kilatini Jeroboam) alikuwa mwana wa Nebati akatawala kwa miaka 22 Ufalme wa Israeli baada ya makabila 10 ya kaskazini kuasi ukoo wa Daudi wakati wa mjukuu wake Rehoboamu.
Biblia inamhukumu hasa kwa kuanzisha sera ya kidini iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi