Yvonne Chaka Chaka
mwanamuziki kutoka Afrika Kusini / From Wikipedia, the free encyclopedia
Yvonne Chaka Chaka (jina la kuzaliwa Yvonne Machaka; mwaka 1965) ni mwimbaji kutoka Afrika ya Kusini.
Aliitwa "Malkia wa Afrika", Chaka Chaka amekuwa mstari wa mbele katika muziki maarufu wa Afrika Kusini kwa miaka 20. Nyimbo kama "I'm Burning Up", "I'm in Love With a DJ", "I Cry for Freedom", "Makoti", "Motherland" na itakayopendwa milele Umqombothi ("Pombe Ya Afrika") zilihakikisha umaarufu wa Yvonne.
Moja ya nyimbo zake pia hutokea katika ufunguzi wa filamu ya mwaka 2004 Hotel Rwanda.