Uafrocentriki

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Uafroncentriki (kutoka Kiingereza: Afrocentrism vilevile huitwa Afrocentricity) ni itikadi ya kitamaduni au mtazamo wa kilimwengu ambao hasa ulitolewa na wasomi Weusi wanaoishi nchini Marekani na imejikita katika kuelezea historia ya mtu mweusi Ni majibu yaliyotokana na toleo la ulimwengu la (Eurocentriki) kuhusu Watu wa Afrika na michango yao kihistoria na vilevile katika kutaka kujua asili yao na itikadi zao. Afrocentricity inajishughulisha hasa elimu ya kujitambua kusimama kama wakala wa Afrika na itakadi nzima ya Pan-African na utamaduni wake, falsafa, na historia.[1][2] Vilevile Afrocentric hutazamiwa kama mawazo ya Wasomi wa Kiafrika na kwingineko ambao walisoma huko Ulaya. Wengi wao waliibuka katika karne ya 20 hasa kipindi kile cha harakati za kupigania uhuru na ukoloni barani Afrika. Kwa mujibu wa wasomi hao, sababu zilizopelekea Unyang'anyi wa Afrika ni kwa sababu ya mapinduzi ya viwanda ambayo yalichukua nafasi barani Ulaya katika karne ya 19. Mapinduzi hayo yalikuwa na changamoto mbalimbali kwa mataifa ya Ulaya. Ili kuondoa changamoto hizo, wakaona bora waje Afrika - jambo ambalo lilipelekea kuigawa Afrika kwa mataifa yenye nguvu ya Ulaya.

Remove ads

Matatizo ya mapinduzi ya viwanda

Yafuatayo ni matatizo au nadharia kulingana na wasomi hao wa Kiafrika walioanisha na kuaminika ndio hasa yaliyowafanya Wazungu waje Afrika:

Uzalishaji wa ziada

Uzalishaji wa kupita kiasi ulisababishwa na matumizi ya mashine badala ya binadamu. Utumiaji wa uliongeza uzalishaji na kupelekea upungufu wa malighafi barani Ulaya. Hivyo basi walilazimika kuja Afrika ili kutatua tatizo hilo la malighafi. Hili lilipeleka unyang'anyi wa Afrika.

Uteja duni

Baada ya mapinduzi ya viwanda, kulikuwa na upungufu wa watu kununua bidhaa za viwandani. Jambo hili lilifanya waje Afrika kutafuta masoko. Vilevile baada ya mapinduzi ya viwanda, sehemu kubwa ya watu walikuwa hawana ajira hivyo upatikanaji wa pesa ukawa mdogo mno, wapi pa kuuzia bidhaa zao, Afrika.

Remove ads

Jisomee

  • The Case against Afrocentrism, Tunde Adeleke (ISBN 1604732938)
  • Afrotopia: The Roots of African American Popular History (Cambridge Studies in American Literature and Culture), Wilson Jeremiah Moses (978-0521479417)

Tazama pia

  • Falsafa ya Afrika
  • Mwamko wa Afrika

Marejeo

Fasihi

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads