Bahari ya Siberia Mashariki

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bahari ya Siberia Mashariki
Remove ads

Bahari ya Mashariki ya Siberia (rus. Восто́чно-Сиби́рское мо́ре vostochno-sibirskoye more) ni bahari ya pembeni ya Bahari ya Aktiki, kaskazini kwa Urusi. Eneo lake ni 944.600 km².

Thumb
Bahari ya Mashariki ya Siberia
Thumb
Pevek ni bandari kuu kwenye bahari ya Mashariki ya Siberia, picha ilipigwa wakati wa mwezi wa Januari 2008

Iko kati ya visiwa vya Siberia Mpya upande wa magharibi na Kisiwa cha Wrangel kwa mashariki upande wa kaskazini ya pwani la Siberia, kati ya Bahari ya Laptev na Bahari ya Chukchi.

Kati ya tabia zake ni tabianchi baridi sana, maji yenye chumvi kidogo, uhaba wa uoto, wanyama na wakazi wa kibinadamu, uwingi wa barafu inayoyeyuka kwenye miezi ya Agosti – Septemba pekee.

Wakazi asilia walikuwa makabila ya kienyeji wawindaji, wavuvi na wafugaji wa reindeer. Leo hii walio wengi ni Warusi. Kazi yao inapatikana hasa katika migodi na kama mabaharia. Mji mkubwa ni bandari la Pevek ambayo ni mji kaskazini zaidi ya Urusi bara mwenye wakazi 4,721.[1][2][3][4][5].

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads