Baraste kuu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Baraste kuu
Remove ads

Baraste kuu (ing. motorway, freeway, au expressway) ni aina ya barabara pana yenye pande mbili zinazotenganishwa na kila upande magari hufuata mwelekeo moja tu. Kila upande huwa na vichororo viwili au zaidi. Baraste kuu ni aina ya barabara inayowezesha motokaa mengi kusafiri kwa kasi kubwa. Hakuna mikingamano inayozuia mwendo. Kama barara nyingine inakata au baraste mbili zinakutana kuna madaraja na njia za kando ambako motokaa inaweza kuongeza kasi yake hadi kuingia kati ya magari mengine.

Thumb
Baraste kuu nchini Marekani yenye vichororo vitano kila upande
Thumb
Kukutana kwa baraste kuu mbili

Hairuhusiwi kusimama au kupumzika kwenye vichororo vya baraste kuu isipokuwa kwenye nafasi kando ya njia iliyotengwa kwa dharura na maeneo ya pekee yaliyotengwa kwa kuegeshea magari.


Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads