California

jimbo la Marekani From Wikipedia, the free encyclopedia

California
Remove ads

California (/ˌkælɪˈfɔːrnjə/) ni jimbo katika Mkoa wa Magharibi wa Marekani linalopatikana kwenye Pwani ya Pasifiki. Linapakana na Oregon upande wa kaskazini, Nevada na Arizona upande wa mashariki, na linashiriki mpaka wa kimataifa na imbo la Mexico la Baja California upande wa kusini. Pamoja na zaidi ya watu milioni 39 wanaoishi kwenye eneo la maili za mraba 163,696 (km² 423,970), ni jimbo lenye idadi kubwa zaidi ya watu Marekani, la tatu kwa ukubwa kwa eneo, na kitengo cha idadi ya watu kikubwa zaidi kisichokuwa cha taifa barani Amerika Kaskazini.

Ukweli wa haraka California, Jimbo ...


Wakazi wamekadiriwa kuwa 39,512,223 mwaka 2019.

California ni kati ya majimbo ya Marekani yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi. Kama California ingekuwa nchi huru ya kujitegemea uchumi wake ungekuwa na nafasi ya 8 duniani. Utalii, kilimo na viwanda vya ndege huajiri watu wengi. Kampuni za kompyuta zimestawi vizuri sana California, kwa mfano Microsoft. Los Angeles, hasa eneo la Hollywood, ni kitovu cha kupiga picha za filamu.

Mji mkuu ni Sacramento. Kuna miji 59 yenye wakazi zaidi ya lakhi moja:

Mji Wakazi
1 Los Angeles 3.957.875
2 San Diego 1.305.736
3 San Jose 944.857
4 San Francisco 799.263
5 Fresno 500,017
6 Long Beach 491.564
7 Sacramento 452.959
8 Oakland 412.318
9 Santa Ana 351.697
10 Anaheim 345.317
Thumb
Hifadhi ya Redwood
Thumb
Mlima Shasta
Thumb
Thumb
Thumb
Yosemite National Park
Thumb
Remove ads

Viungo vya nje

Ukweli wa haraka


Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu California kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads