Carrie-Anne Moss

From Wikipedia, the free encyclopedia

Carrie-Anne Moss
Remove ads

Carrie-Anne Moss (amezaliwa tar. 21 Agosti 1967) ni mshindi wa Tuzo ya Guild akiwa kama mwigizaji bora filamu wa kike kutoka nchini Kanada. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa jina la Trinity kutoka katika mfululizo wa filamu za Matrix, vilevile Natalie kutoka katika filamu ya Memento.

Ukweli wa haraka Carrie Anne Moss ...
Remove ads

Wasifu

Maisha ya awali

Carrie-Anne Moss alizaliwa mjini Burnaby, British Columbia. Pia ana kaka yake mkubwa aitwaye Brooke. Mama yake na Moss (Bi. Barbara) alimwita mwanae jina la Carrie Anne, kwakuwa Moss alizaliwa wakati wa kibao maarufu cha The Hollies cha mwaka wa 1967, kilikwenda kwa jina la "Carrie-Anne" hivyo mama kwa mapenzi yake akaamua kumwita mwanawe jina hilo la wimbo.

Akiwa yungali mdogo, Moss aliishi na mama yake mjini Vancouver, baada ya wazazi wake kutarikiana. Akiwa na umri wa miaka kumi na moja, Moss akajiunga na kikundi cha muziki cha watoto cha mjini Vancouver, na baadaye kuelekea katika safari za kimuziki wa kwaya katika nchi za Ulaya.

Miaka ya baadaye alielekea zake nchini Marekani na kuweza kujiunga na moja kati ya shule za sanaa iliyopo mjini Pasadena. Mwaka wa 1985, alirudi tena mjini Vancouver na akabahatika kuwa mwanamitindo. Kazi hiyo ya uwanamitindo ilipelekea kumsafarisha katika nchi ya Japan na Hispania kunako miaka ya 1980.

Remove ads

Maisha binafsi

Moss ameolewa na Bw. Steven Roy kunako mwaka wa 1999, ambaye pia ni mwigizaji wa filamu. Wawili hao wamebahatika kupata watoto wawili wa kilume, wa kwanza amezaliwa mwishoni mwa mwaka wa 2003 na wa pili amezaliwa mnamo mwezi Novemba katika mwaka wa 2005. Moss, yumakini sana katika kuitunza familia yake na mwenyewe pia. Moss pia ana mtoto mkubwa ambaye anajulikana kwa jina la Owen.

Na rafiki mkubwa wa Moss ni mwigizaji mwenzi anajulikana kwa jina la Maria Bello, ambaye ndiye mama mlezi wa mtoto wa kwanza wa Moss.

Remove ads

Filamu alizoigiza

Maelezo zaidi Mwaka, Jina la filamu ...

Filamu za katika televisheni

Maelezo zaidi Mwaka, Jina la filamu ...

Tuzo alizoshinda na utambulisho

Marejeo

  1. Carrie-Anne Moss - Profile, Latest News and Related Articles

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads