Mgongo wa bahari wa Chile
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mgongo wa bahari wa Chile (kwa Kiingereza: Chile Ridge) ni mgongo wa baharini yaani safu ya milima kwenye sakafu ya bahari. Unafuata mpaka baina ya mabamba mawili ya gandunia: bamba la Nazca na bamba la Antaktiki.

Mgongo wa bahari wa Chile unazama chini ya bara la Amerika Kusini kwenye mfereji wa Peru-Chile unaoitwa pia mfereji wa Atamaca. [1]
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads