Dado
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dado (pia: Audoin, Audoen, Owen na Ouen wa Rouen; Sancy, Ufaransa, 609 – Clichy, Ufaransa, 686)[1][2][3] alikuwa waziri wa Wafaranki na halafu askofu.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.
Maisha
Mtoto wa mtakatifu Authaire (Audecharius), alilelewa katika ikulu ya mfalme Chlothar II (aliyefariki 629), ambapo alipata elimu na uanajeshi pamoja na vijana wengine wa koo maarufu.
Baadaye alisimamia mali ya Dagobati I[5], akishika sana maadili[6] na akiwa na marafiki kama watakatifu Wandrili, Didier wa Cahors na Eligius wa Noyon, ambaye Dado aliandika habari za maisha yake.
Mwaka 635 pamoja na ndugu zake Ado na Rado alianzisha abasia ya Rebais, halafu monasteri ya Mt. Wandrili huko Rouen, na nyingine ya kike huko Fécamp.
Mwaka 641 alifanywa askofu wa Rouen, jimbo aliloliongoza vizuri kwa miaka 43, akijenga makanisa na monasteri.[5][7]
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads