Erasmus wa Rotterdam

From Wikipedia, the free encyclopedia

Erasmus wa Rotterdam
Remove ads

Desiderius Erasmus wa Rotterdam (Rotterdam, leo nchini Uholanzi, 27 Oktoba[1] 1466Basel, leo nchini Uswisi, 12 Julai 1536), anayejulikana kifupi kama Erasmus tu, alikuwa Mholanzi aliyechangia sana tapo la Renaissance[2], pia padri na mwanateolojia wa Kanisa Katoliki aliyehimiza urekebisho wake.

Thumb
Desiderius Erasmus mwaka 1523 alivyochorwa na Hans Holbein the Younger.

Erasmus alikuwa msomi mkubwa aliyeweza kuandika kwa Kilatini fasaha. Akitumia mbinu za kitaalamu aliandaa matoleo mapya ya Agano Jipya kwa lugha hiyo na kwa Kigiriki.

Mafundisho yake mbalimbali, yaliyojitokeza katika vitabu maarufu, yaliandaa mwanzo na uenezi wa Uprotestanti, ingawa mwenyewe alikataa kuuunga mkono.[3][4]

Erasmus alifariki ghafla Basel mwaka 1536.[5]

Remove ads

Maandishi yake

  • Novum Instrumentum omne
  • Colloquia
  • Apophthegmatum opus
  • Adagia
  • Copia: Foundations of the Abundant Style (1512) (a.k.a. De Copia)
  • The Praise of Folly
  • The first tome or volume of the Paraphrase of Erasmus vpon the newe testamente
  • A playne and godly Exposytion or Declaration of the Commune Crede
  • A handbook on manners for children
  • Disticha de moribus nomine Catonis
  • The Education of a Christian Prince (1516)
  • Bellum (essay, 1517)
  • De recta Latini Graecique Sermonis Pronunciatione (1528)
  • De pueris statim ac liberaliter instituendis (1529)
  • De octo orationis partium constructione libellus (1536)
Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads