Freetown
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Freetown ni mji mkuu pamoja na bandari kubwa na kitovu cha uchumi wa nchi ya Sierra Leone. Uko kando ya Atlantiki kwenye rasi ya Freetown. Idadi ya wakazi ni 1,070,000.

Historia
Mji uliundwa mwaka 1787 kwa ajili ya watumwa wenye asili ya Afrika waliowekwa huru. Ndiyo asili ya jina "Freetown" linalomaanisha "Mji wa watu huru".
Ulikuwa mji mkuu wa koloni la Uingereza katika Afrika ya Magharibi kati ya miaka 1808 hadi 1874.
Hadi leo Wakreoli ambao ni wazao wa watumwa waliopewa uhuru kama walowezi ni tabaka la pekee Freetown wakionekana kwa utamaduni na lugha ya pekee.
Katika miaka ya 1990 mji ulikuwa mahali pa mapigano kati ya wanamgambo na askari za ECOWAS.
Remove ads
Uchumi
Uchumi wa Freetown unategemea hasa bandari. Kuna pia viwanda vya sigara, vya kutengeneza petroli, vya chakula na za kusafisha almasi.
Tazama pia
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Freetown kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads