Gertrudi wa Thuringia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Gertrudi wa Thuringia
Remove ads

Mtakatifu Gertrudi (pia: Getrudi Mkuu; 125617 Novemba 1301) alikuwa mmonaki wa kike wa monasteri ya Helfta nchini Ujerumani.

Thumb
Gertrudi wa Thuringia

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira. Heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Inosenti XI mwaka 1677.

Sikukuu yake ni tarehe 16 Novemba[1].

Maisha

Gertrudi alizaliwa katika mji wa Eisleben, mkoa wa Thuringia, nchini Ujerumani mwaka 1256.

Katika utoto wake alilelewa na watawa wa kike Wabenedikto (labda wa urekebisho wa Citeaux) huko Helfta, ambako alifaulu vizuri katika masomo yake, hasa falsafa, historia na fasihi, pamoja na kukimbilia upwekeni kwa juhudi zenye ari.

Baada ya kumuongokea kabisa Mungu na kujiweka kabisa mikononi mwake, alijiunga na monasteri hiyo, alipofuata vizuri ajabu njia ya ukamilifu, ajitosa katika kusali na kufanya fikara kwa kumkazia macho ya imani Kristo msulubiwa [2].

Alifariki tarehe 17 Novemba 1301.

Remove ads

Sala zake

Mungu, unayestahili upendo usio na mipaka, sina chochote cha kupimia vema ukuu wako, lakini hamu yangu kwako ni hivi kwamba, kama ningekuwa na yale yote uliyonayo wewe, ningekupa yote kwa furaha na shukrani.


Kwa ajili ya uongofu nakutolea, Baba mpenzi sana, mateso yote ya Mwanao mpendwa sana tangu wakati ule ambapo, akilazwa horini juu ya nyasi, alianza kulia, halafu akavumilia mahitaji ya utoto, mapungufu ya ubalehe, mateso ya ujana, hadi alipoinamisha kichwa akafa msalabani kwa mlio mkubwa.

Vilevile, kwa kufidia makosa yangu ya uzembe, nakutolea, Baba mpenzi sana, mwendo wote wa maisha matakatifu sana ambayo Mwanao pekee aliyaishi kikamilifu kabisa katika mawazo, maneno na matendo yake tangu atumwe kutoka ukuu wa kiti chako cha enzi kuja katika dunia yetu, hadi alipouonyesha mtazamo wako wa Kibaba utukufu wa mwili wake mshindi.

Kama shukrani nazama katika kilindi kirefu sana cha unyenyekevu, na pamoja na huruma yako isiyolipika, nasifu na kuabudu wema wako mtamu sana.

Wewe, Baba wa huruma, nilipokuwa ninapoteza maisha yangu hivyo, ulikuza kwangu mawazo ya amani, si ya mabaya, ukaamua kuniinua kwa wingi na ukuu wa fadhili zako.

Kati ya mengine, ulitaka kunijalia ujirani usiothaminika wa urafiki wako kwa kunifungulia kwa namna mbalimbali hazina ile azizi sana ya umungu, ambayo ni moyo wako wa Kimungu, na kwa kunitolea kwa wingi mkubwa kila utajiri wa furaha ndani yake.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads